PSSSF Kanda ya Kusini yawanoa Wanahabari

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ( PSSSF) Kanda ya kusini unaosimamia Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma umewanoa waandishi wa habari mkoani Mtwara kwa kutoa mafunzo kuhusu namna bora ya kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa mfuko huo.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa PSSSF Kanda ya Kusini Lulyalya Sayi amesema wameona upo umuhimu mkubwa wa kutoa elimu hiyo kwa wanahabari hao ili kujenga mahusiano, mafunzo yaliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Pia amesema elimu kwa wanahabri niĀ  ili wafahamu faida za mfuko pamoja na majukumu yake na waweze kufanya kazi hiyo kikamilifu ya kuhabarisha jamii masuala mbalimbali ya mfuko.

Mada za mafunzo ni pamoja na matumizi ya mfumo wa PSSSF kidigitali unaomwezesha mwanachama kuomba mafao yake kupitia mtandao, kujisajili mwanachama mpya sambamba na kufuatia maendeleo ya akaunti ya mwanachama.

“Nitoe wito kwa baadhi ya waajiri wanaodaiwa na PSSSF kulipa fedha kwa wakati ili madeni hayo yasikwamishe mafao kwa wanachama na sisi PSSSF tutimize wajibu wa kuwalipa wanachama kwa wakati,”amesema Sayi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mtwara (MTPC) Grace Kasembe ameishukuru PSSSF kwa kuona umuhimu wa kuleta mafunzo hayo kwa wanahabari huku akiahidi kuwa mabalozi wazuri kwa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa mfuko.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button