PSSSF wapewa tuzo kufanikisha mkutano TAPSEA

ARUSHA: MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepokea tuzo kutoka kwa Makamu wa Rais, Philip Mpango ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa mfuko huo katika kufanikisha Mkutano Mkuu  wa 12 wa Chama cha Waandishi Waendesha Ofisi (TAPSEA) uliofanyika Arusha.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Meneja Utawala PSSSF, Fatma Chondo amesema ni jambo la furaha kwa mfuko kupata tuzo hiyo na kuahidi kwamba PSSSF itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau wote ili kuhakikisha kunakuwepo na maendeleo endelevu katika sekta ya hifadhi ya jamii.

Aidha katika mkutano huo PSSSF imeendelea na zoezi la kuchukua alama za vidole kwa wanachama wake wanaoshiriki mkutano huo.

Zoezi hilo linaendeshwa nchi nzima ambapo watumishi wa PSSSF wanapita kwenye maeneo ya kazi na kufanya kazi hiyo kwa lengo la kuboresha taarifa na kurahisisha huduma kwa wanachama.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button