Putin agoma kufanya mazungumzo na Zelensky

URUSI : RAIS wa Urusi, Vladimir Putin, amesema nchi yake iko tayari kufanya mazungumzo ya amani na Ukraine, lakini amekataa kufanya mazungumzo moja kwa moja na Rais Volodymyr Zelensky, ambaye amemuita kuwa si mtu wa ukweli katika matamshi yake.

Rais Zelensky ameonyesha kukerwa na kauli za Putin, akisema kuwa kiongozi huyo wa Urusi anahofia mazungumzo na kutumia mbinu za kijinga ili kurefusha mgogoro wa kivita ambao umedumu kwa karibu miaka mitatu.

Aidha, Rais wa Marekani, Donald Trump, ameweka vikwazo kwa pande zote mbili kutafuta amani, akilazimisha mapigano kusitishwa tangu alipoingia madarakani Januari 20.

Trump amesema kuwa Zelensky yuko tayari kwa mazungumzo ya amani, huku akitishia vikwazo vikali dhidi ya Urusi. SOMA: Nitamaliza vita vya Urusi na Ukraine – Trump

Putin amesisitiza kuwa, kama Rais Zelensky atataka kushiriki katika mazungumzo, atawatuma wawakilishi watakaomuwakilisha katika majadiliano, huku akiongeza kuwa Zelensky si rais halali kwa sababu muhula wake wa urais ulimalizika wakati wa sheria ya kijeshi.

Kwa upande wake, Zelensky amesema kuna fursa ya kufikia amani ya kweli, lakini Putin anahujumu juhudi za kusitisha mapigano na kufikia muafaka.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button