Urusi inahaki kutumia silaha za nyuklia

URUSI: RAIS wa Urusi, Vladimir Putin amesema kuwa Urusi ina haki ya kutumia silaha za nyuklia dhidi ya nchi yoyote itakayoleta tishio dhidi yake.

Akizungumza katika mkutano wake wa kila mwaka na vyombo vya habari, Putin alisema, “Tunazungumzia vitisho vya kijeshi vinavyoibuka, kama vile kuibuka kwa mifumo ya kupambana na makombora.”

Kauli hii inakuja mwezi mmoja baada ya Kremlin kuidhinisha mabadiliko ya kanuni mpya kuhusu utumiaji wa silaha za nyuklia. SOMA : Jeshi la Urusi lateka vijiji viwili Ukraine

Advertisement

Kanuni hizo mpya zinasema kuwa, shambulio kutoka taifa lisilo na silaha za nyuklia, ikiwa litafanyika kwa msaada wa nchi yenye nguvu za nyuklia, litachukuliwa kama shambulio la pamoja dhidi ya Urusi.