Putin yuko tayari kukutana na Trump

MAREKANI : RAIS mteule wa Marekani Donald  Trump amethibitisha Rais wa Urusi, Vladmir Putin yuko tayari kuzungumza kuhusu kusitisha vita vya Urusi na Ukraine.

“ Ni kweli Rais Putin anataka kukutana  na mimi” alisema  Trump  katika kongamano huko Arizona nchini Marekani. SOMA: Trump ajitapa kumaliza vita vya Urusi, Ukraine

“Itabidi tusubiri lakini lazima tukomeshe vita hivi. Vita hivi vinatisha, vinatisha.”Alisema Trump.

Advertisement

Trump, ambaye anatarajia kurudi Ikulu ya White House mwezi Januari 2025, ambaye katika kampeni zake aliahidi kumaliza  vita vya Urusi na Ukraine.

Hivi karibuni Trump pia alikosoa uidhinishaji wa Biden kwa Ukraine kutumia silaha za masafa marefu zilizotolewa na Marekani kushambulia eneo la Urusi.

“Idadi ya wanajeshi waliouawa.Ni ardhi tambarare, na risasi zinapaa, risasi zenye nguvu, bunduki zenye nguvu, na kitu pekee kinachoweza kuzuia ni mwili wa binadamu,” Trump alisema, akisisitiza kwamba vita vya Ukraine visingefanyika iwapo angekuwa rais wa Marekani wakati huo.