QATAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa nchi wa Qatar anayeshughulikia masuala ya Nishati Saad bin Sherida Al- Kaabi.
Mazungumzo hayo yametoa nuru kwa Qatar kuiuzia Tanzania mbolea aina ya Urea kwa gharama nafuu.
Kikao hiki pia kilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Habib Awesi Mohammed pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea ( TFC ) Samwel Ahadi Mshote.
Hapo kesho, Rais Dk. Mwinyi anatarajiwa kushiriki mkutano mkubwa wa Kimataifa wa kutimiza miaka 30 ya Familia Duniani utakaofanyika jijini Doha.
Mkutano huu unafanyika kufuatia Azimio la mwaka 1994 la Umoja wa Mataifa la Mwaka wa Kimataifa wa Familia ( IYF ) lililopitishwa rasmi na Baraza la Umoja wa Mataifa likizingatia thamani na umuhimu uliopo wa kuzilinda na kuzisaidia familia kupitia sheria za Kimataifa.
SOMA : Mweli: Matumizi ya mbolea yafikia tani laki nane nchini