VENEZUELA : WAZIRI wa Mambo ya Ndani nchini Venezuela, Diosdado Cabello amesema wamewakamata raia saba wa kigeni kwa tuhuma za kula njama juu ya kile ambacho kinadaiwa kuwa ni njama ya kumuua Rais Nicolás Maduro.
Akitoa taarifa hiyo katika bunge la Venezuela, Waziri Cabello amesema raia mmoja wa Marekani alikamatwa mjini Caracas wakati akichukua picha za mifumo ya umeme, vifaa vya mafuta na vifaa vya kijeshi.
Wiki iliyopita, raia sita wengine wa kigeni walikamatwa ambapo watatu kutoka Hispania, wawili kutoka Marekani na raia mmoja kutoka Jamhuri ya Czech.