Congo waandamana kupinga wizi wa madini

CONGO: MAMIA ya watu wameamua kuandamana nchini DR CONGO kupinga uchimbaji haramu wa madini unaoendelea katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa zinasema kuwa uchimbaji wa madini unaofanyika katika eneo hilo, umekuwa ni haramu kwa sababu makampuni ya kichina mengi yamekuwa yakichimba bila ya kuwa  na vibali maalum.

Maandamano hayo yamefuatia tangazo la Jumapili la kuwakamata raia watatu wa China waliokutwa na dhahabu pamoja na pesa nyingi taslimu, kwa mujibu wa gavana wa Kivu Kusini Jean Jacques Purusi.

Maafisa hao wamekiri mamia ya makampuni ya uchimbaji madini na hasa ya Wachina, yanachimba dhahabu bila ya kuonesha faida wanazopata kwa vyombo husika na mara nyingi shughuli hizo hufanywa bila ya vibali halali. SOMA: Bil 30/- za EU kunufaisha wachimbaji wadogo madini

 

Chanzo: Dw

 

Habari Zifananazo

Back to top button