Raia Gaza waingia hofu kusitishwa UNRWA

PALESTINA : RAIA wanaoishi katika ukanda wa Gaza wanahofu juu ya upatikanaji wa misaada ya kibinadamu baada ya Israel kusitisha UNRWA kutoa huduma katika ukanda huo.

Hii leo wabunge wa Israel wamekutana kutunga mswada wa sheria utaodhibiti Shirika la Umoja wa Mataifa  UNRWA kufanya shughuli zake katika ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya Israel.

Uamuzi wa kuzuia Unrwa kufanya kazi huko Gaza ni mbaya kwa sababu tunapata chakula kupitia wao na watoto wetu wanasomeshwa katika shule zao.

“Elimu ni jambo muhimu zaidi. Natumai uamuzi huu hautatekelezwa kwa sababu sio sahihi.” Walisema wapalestina wanaoishi Gaza.

SOMA : Jeshi la Israel laua wapalestina 11

Hatahivyo, Umoja wa Mataifa umesikitishwa na hatua hiyo ya uundwaji wa mswada wa sheria utakaoipinga  UNRWA kufanya  shughuli katika ukanda wa Gaza na kusema kuwa  UNRWA itaendelea kufanya shughuli zake kuwasaidia  wapalestina.

Habari Zifananazo

Back to top button