PALESTINA : JESHI la Israel limeshambulia eneo lenye uhitaji wa misaada ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza na kuwaua Wapalestina 11.
Shambulio hili limefanyika wakati jeshi hilo likipeleka magari ya kivita katika eneo la kaskazini la Jabalia wakati eneo hilo likiwa na hitaji kubwa la chakula.
Baadhi ya raia wa Jabalia wamesema jeshi la Israel limelipua nyumba kadhaa kwa mashambulizi ya angani, mizinga na kutega mabomu katika majengo.
Hatahivyo , vikosi vya uokoaji katika eneo hilo wamesema watu kadhaa wamejeruhiwa ambao walijificha katika shule moja iliyoshika moto baada ya kushambuliwa na kombora la Israel.
Kufuatia shambulio hilo, Jeshi la Israel limekubali kuruhusu malori 50 ya msaada kuingia kaskazini mwa Gaza.
Wakati huo huo, jeshi la Syria limedai kuwa Israel imewajeruhi raia wawili na kuharibu kambi ya kijeshi mapema leo katika shambulizi lililofanywa kwenye mji wa pwani wa Latakia nchini humo.