MAREKANI : WAKATI Wananchi wa Marekani wakiendelea kusikiliza sera za Wagombea,Rais Joe Biden amevunja ukimya na kuwajibu wafuasi wa Republican kuhusu matamshi ya neno “takataka”.
Akizungumza na wapiga kura kwa njia ya mtandao wa Zoom, Rais Biden ameweza kubainisha mambo mengi mazuri yanayohusu watu wanaoishi katika Kisiwa cha Puerto Rico.
“Naweza kusema watu wanaoishi Puerto Rico ni watu wazuri na wenye heshima,” Biden amesema.
Kisha hakusita kuwajibu wafuasi wa Republican.
“Takataka pekee ninayoiona mimi iko huko nje, wafuasi wa kilatino wanatumiwa vibaya, na hii haikubaliki.” Alisema.
Licha ya kulitolea ufafanuzi kuhusu neno “takataka”, wafuasi wa Republican wameendelea kusema neno hilo liliwalenga wafuasi wa Trump.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Ikulu ya White house imefafanua kuwa neno hilo takataka lilimlenga mchekeshaji mmoja aliyeshambulia Puerto Rico na sio kundi la watu.