Rais Dk. Mwinyi aipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BOT)

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Mafanikio  ya Ukuaji wa Uchumi wa Tanzania Unatokana  na Usimamizii Mzuri  wa Uchumi unaofanywa na Benki kuu ya Tanzania (BoT).

Rais Dkt, Mwinyi amesema hayo  alipojumuika katika Futari ya Pamoja ilioandaliwa na Benki hiyo katika Hoteli ya Madinat Al Bahr, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 25 Machi 2025.

Aidha Rais Dkt, Mwinyi amesema amekuwa akifarijika na Ushauri wa Kifedha anaoupata kutoka Benki Kuu katika kusimamia Uchumi wa Zanzibar.

Advertisement

 

Amebainisha kuwa  Mafanikio  Makubwa yanayopatikana hivi sasa  kwa Uchumi wa Tanzania ikiwemo Zanzibar yamechangiwa na   Uimara wa Usimamizi Bora wa Kifedha unaotekelezwa na BoT.

Halikadhalika Rais Dkt, Mwinyi ameipongeza BoT kwa Kuendeleza Utaratibu wa Kuwakutanisha pamoja Wadau wa Benki hiyo kila Mwaka wakati wa  Mwezi wa Ramadhani.

Naye Gavana wa Benki kuu ya Tanzania  Emmanuel Mpawe Tutuba  amemuhakikishia Rais Dkt, Mwinyi kuwa Uchumi wa Tanzania Uko Vizuri na unaendelea kukua na Sekta ya  Fedha inafanya Vizuri na Mfumuko wa bei  upo Mdogo .

Amefahamisha kuwa Uchumi wa Tanzania Bara umekuwa kwa Asilimia 5.4 na Zanzibar umekuwa kwa Asilimia 7. SOMA: BoT yanunua tani mbili za dhahabu

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *