Dk. Mwinyi atunukiwa shahada ya heshima

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Shahada ya  Heshima ya Uzamivu  ya Chuo Kikuu cha Zanzibar.

Chuo Kikuu cha Zanzibar kimemtunuku  Shahada hiyo ikiwa ni kutambua   na kuthamini Mchango  wa Uongozi wake  Unaoacha Alama  na historia itakayokumbukwa  wakati wote.

Hafla ya kutunukiwa Shahada hiyo imefanyika leo tarehe 5 Disemba 2024 katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu wakati wa Mahafali ya 22 ya Wahitimu wa mwaka 2024

Advertisement

Shahada hiyo ya Heshima ya Uchumi  ametunukiwa kuthamini Mchango wake na Mafanikio makubwa yaliofikiwa Zanzibar hususan  Ukuaji wa Uchumi    na Maendeleo yaliyopatikana katika kipindi kifupi cha uongozi wake wa miaka minne.

Rais Dk Mwinyi amekishukuru Chuo hicho kwa kuthamini juhudi na kazi anazofanya kwa ajili ya Maendeleo ya nchi. SOMA: SMZ kuendelea kuifungua Pemba

Aidha Rais Dk.Mwinyi  amebainisha kuwa  Shahada hiyo aliotukuwa Inaakisi kazi nzuri inayoifanya na Serikali anayoiongoza na itamuongezea hamasa ya Maendeleo zaidi.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameahidi kuienzi heshima hiyo  na kuwahakikishia wananchi kuendelea  kuwatumikia kwa uwezo wake wote na sio mwisho wa safari bali mwanzo wa hatua kubwa ya maendeleo yajayo.