Rais Museveni, Ruto na Hassan wawasili Tanzania

Mkutano huu wa Wakuu wa Nchi za EAC umefuatiwa na tukio maalum la maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, likiwa na kaulimbiu, “Miaka 25 ya EAC : Safari ya Tafakuri na Dira ya Baadaye.”
Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto, amewasili Tanzania leo, Novemba 29, kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), unaofanyika Arusha Novemba 29 na 30.

ARUSHA – Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto, na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, wamewasili Tanzania leo, Novemba 29, kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), unaofanyika Arusha.

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania tayari yupo Arusha kwa kikao hicho amacho kimeshuhudia matukio mengi ya kihistoria.

Viongozi hao wamewasili wakitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kupokelewa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Omar Said Shaaban. 

Advertisement

Rais Ruto alipokelewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, huku Rais Hassan Sheikh Mohamud akipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dennis Londo.

Mkutano huu wa Wakuu wa Nchi za EAC umefuatiwa na tukio maalum la maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, likiwa na kaulimbiu, “Miaka 25 ya EAC : Safari ya Tafakuri na Dira ya Baadaye.”

Rais Ruto alipokelewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi.
Rais Ruto alipokelewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi.

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, amewasili Tanzania leo, Novemba 29, 2024, kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), unaofanyika Arusha Novemba 29 na 30.

Image
Rais Museveni alipokelewa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Omar Said Shaaban.

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Somalia, Hassan Sheikh Mohamud,
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, amewasili Tanzania leo, Novemba 29, kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), unaotarajiwa kufanyika Arusha Novemba 29 na 30.

Image
Rais Hassan Sheikh Mohamud alipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dennis Londo.