Rais Mwinyi afungua majengo ya Mahakama

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amezindua rasmi majengo mapya ya Mahakama za Mikoa na Wilaya Mazizini, Mkoa Mjini Magharibi, leo tarehe 8 Septemba 2025.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali ina mpango maalum wa kujenga majengo ya Afisi za Serikali, Baraza la Wawakilishi na Mahakama ili kuimarisha uwajibikaji na utoaji wa huduma bora.SOMA: Mahakama Yaruhusu Uteuzi Mpya wa IEBC
Halikadhalika, Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa kukamilika kwa Mahakama hizo ni mwanzo wa mradi mwingine chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia, utakaohusisha ujenzi wa Mahakama tano pamoja na Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki.

Kwa upande mwingine, Rais Mwinyi ametoa wito kwa watendaji wa Mahakama kutunza miundombinu hiyo na ameipongeza Mahakama ya Tanzania na Kampuni ya CRJE–East Africa kwa kazi nzuri ya usanifu na ujenzi wa majengo hayo ya kisasa.



