Rais Mwinyi ahudhuria Kongamano la ‘Light Upon Light’

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewasili katika Uwanja wa New Amaan Complex Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja uhudhuria Kongamano la Kimataifa la ‘Light Upon Light.’

Advertisement

Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini, pamoja na watoa mada mashuhuri akiwemo Mufti Menk kutoka Uingereza, Sheikh Muhammad Saleh, Sheikh Wael Ibrahim, na Sheikh Ali Hammuda.