Rais Mwinyi akutana na ujumbe wa SEOM

ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amekutana na Ujumbe wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SEOM) Ikulu, Zanzibar.
 
Ujumbe huo unaoongozwa na Spika Mstaafu wa Bunge la Malawi, Richard Msowoya umemueleza Rais Mwinyi kuwa SEOM imejipanga kupeleka wajumbe wake katika maeneo yote visiwani Zanzibar.
 
Aidha, wakiwa Visiwani Zanzibar, ujumbe wa SEOM umekutana na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) pamoja na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button