Rais Mwinyi kufunga maonesho ya 77 kesho

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, kesho Julai 13, 2023 anatarajiwa kufunga Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba 2023’

Maonesho hayo yalianza Mei 28 yakishirikisha wafanyabishara kutoka ndani na nje ya nchi kuonesha bidhaa zao na teknolojia mbali mbali zilizovumbuliwa.

Ratiba inaonesha mgeni rasmi atawasili katika viwanja hivyo kuanzia saa sab ana nusu mchana na atatembelea mabanda mbalimbali kabla ya kwenda kwenye sherehe za kufunga maonesho hayo ambayo yataambatana na ugawaji wa tuzo kwa mabanda yaliyofanya vizuri kipindi chote cha maonesho hayo.

Advertisement

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, Latifa Khamis amesema Maonesho ya wa mwaka huu ‘Sabasaba 2023’ yamefanikiwa kwa asilimia kubwa ya malengo waliyojiwekea.

“Tunaendelea kukusanya taarifa mbalimbali za maonesho haya, lakini kwa kiasi kikubwa maonesho yam waka huu yamekuwa ya mafanikio makubwa kwani yamekutanisha wafanyabiashara mbalimbali kutoka nchi tofauti.

”Amesema na kuongeza

“Kupitia Maonesho haya tumewakutanisha wafanyabiashara wetu na wafanyabiashara kutoka nchi za China, India, Afrika Kusini, Iran na ni matumaini yetu wametengeneza mahusiano ambayo mbeleni yatazaa matunda, tutakwenda kuwa na mikataba mikubwa na yenye manufaa kwetu.”Amesema Latifa

Amesema, pia mafanikio mengine ni kuweza kuandaa siku maalumu ya nchi tatu ambazo ni Iran, China na India ambapo zilifanikiwa na kuweza kufikiwa kwa lengo la kuweza kutangaza fursa zilizopo pia siku maalumu ya Zanzibar ambayo ilielezea vivutio vinavyopatikana katika visiwa vya unguja na Pemba.

3 comments

Comments are closed.