ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar Dk.
HusseinMwinyi amesema Zanzibar ni salama kwa mtu yoyote, ina amani, umoja, mshikamano na utulivu, kuendelea na shughuli za kimaendeleo na ibada.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo akizungumza alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya sala ya Ijumaa na kufungua Ijitimai ya Kimataifa Tabligh Markaz Magome ya siku tatu Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba leo Februari 2, 2024.
Rais Mwinyi amewataka waumini kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano.
Aidha, ametoa wito kwa waumini kuwafundisha watoto elimu ya dini ili wawe na hofu ya Mungu kwa kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na vitendo vya udhalilishaji .
Pia, ameipongeza Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kwa kuratibu vizuri shughuli za dini kwa utulivu, amani na mshikamano