Waziri afutwa kazi tuhuma za ubadhirifu Nigeria

RAIS wa Nigeria, Bola Tinubu amemsimamisha kazi Waziri wa Masuala ya Kibinadamu, Betta Edu na kulitaka shirika linalofuatilia ufisadi kuchunguza miamala ya kifedha inayohusisha wizara yake juu ya madai ya utoroshwaji wa zaidi ya Naira milioni 585 ambazo ni sawa na Sh bilioni 1.6.

Betta Edu, Waziri wa Masuala ya Kibinadamu na Kupunguza Umaskini, ndiye waziri wa kwanza kusimamishwa kazi, chini ya miezi sita baada ya kuteuliwa.

Alisimamishwa kazi Jumatatu kufuatia taarifa mbalimbali za umma kuhusu kashfa hiyo.

Msemaji wa Rais Tinubu, Ajuri Ngelale alisema Rais ameagiza Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha (EFCC) kufanya uchunguzi wa kina kuhusu masuala yote ya shughuli za kifedha zinazohusisha Wizara ya Edu.

Habari Zifananazo

Back to top button