RAIS wa Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri leo April Mosi, 2022
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunua inasema katika mabadiliko hayo, RAIS Samia amemteua Jenista Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).
Mhagama anachukua nafasi ya George Boniface Simbachawene. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Aidha, amemteua George Bonifacellû Simbachawene (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. .
Simbachawene anachukua nafasi ya Jenista Mhagama.
Kabla ya uteuzi huo Simbachawene alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).
Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Aprili, 2023.
Mawaziri wateule wataapishwa kesho Aprili 2, 2023 saa 3 asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam.