Rais Samia afanya uteuzi, Prof Makubi ‘Boss’ mpya Moi

RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Profesa Abel Makubi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI).

Prof. Makubi anachukua nafasi ya Dk Respicious Boniface aliyemaliza muda wake.

Pia, amemteua Dk Edwin Mhede kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB Plc kwa kipindi cha pili.

Katika taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, iliyotolewa leo June 8,2023 Zuhura Yunus amesema Rais Samia pia amemteua Omary Issa kuwa Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM- AIST).

Issa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco anachukua nafasi ya Dk Ghalib Bilal, Makamu wa Rais Mstaafu ambae amemaliza muda wake.

Pia, amemteua Dk Abdulhamid Yahaya Mzee kuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC).

Dk Mzee alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akichukua nafasi ya Dk Marten Lumbanga ambae amemaliza muda wake.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x