Rais Samia aipongeza Simba kwa ushindi

ZANZIBAR: RAIS wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, ameipongeza timu ya Simba ya Dar es Salaam kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini, mmchezo kwa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika uliofanyika Uwanja wa New Amaan Complex.
“Hongera sana kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF Confederation Cup).

“Mmeleta furaha kwa mashabiki wenu na Watanzania wote na kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu. Motisha kutoka kwangu mtaipokea kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ninawatakia kila la kheri,” ameandika Rais Samia kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii.
Kutokana na matokeo hayo Simba sasa inahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo wa marudiano Aprili 27, 2025 nchini Afrika Kusini, itakuwa imetinga hatua ya fainali ya michuano hiyo.



