”Mageuzi ya msingi na muhimu ya kiuchumi, kisiasa na uchaguzi yatahakikisha sheria na haki nchini zinapatikana na ambazo kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakua na kuzalisha ajira kwa watu wake. Mageuzi haya yanapaswa kuimarisha juhudi zetu kuelekea kuwa na jamii yenye haki, kustawi kwa demokrasia na uchumi unaokua kwa faida ya Watanzania wote”, alisema Mhe. Nape alipozungumzia nguzo ya tatu ya mageuzi.
Aidha Nape alizungumzia nguzo ya nne anayotumia Mama samia Suluhu hassan kuwa ni kuijenga upta Tanzania mpya. “Mama Samia, anahakikisha kuwa uchumi unakua ambao utazalisha ajira za kutosha kwa vijana wetu ni muhimu na ya kutosha ya kujenga upya Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania, kama hali ya ustawi wa karne ya 21 inayosisitiza kuwa maendeleo ni uhuru wa msingi.
Ujenzi wa taifa ni mchakato unaohitaji uongozi unaoweza kuimarisha suluhu baini ya wananchi wote”, alimalizia Mhe. nape Nnauye.
Tamasha hilo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro na lilihudhuriwa na viongozi na wananchi mablimbali walioalikwa kuhudhuria. Katika Tamasha hilo, Lady JD pia alizindua Taasisi ya Binti itakayokuwa inahamasisha wanawake na hususani mabinti kusimama imara katika kuleta maendeleo yao bila kujali jinsia zao na kulalamika kuwa hawana nafasi katika shughuli za kujenga Tanzania.