Rais Samia ateua, atengua

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA)
Amemteua Frank Kanyusi  kuwa Kabidhi Wasii Mkuu.
Kabla ya uteuzi Frank alikuwa Mwanasheria Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara.
Frank anachukua nafasi ya  Angela Kemanzi Anatory ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Pia, amemteua Irene Joseph Lesulie kuwa Naibu Kabidhi Wasii Mkuu.
Kabla ya uteuzi Irene alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mashauri ya Kimataifa, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Irene anachukua nafasi ya Lina Robert Sanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa  Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu  Zuhura Yunus iliyotolewa leo Juni 11, 2023  imesema uteuzi huo  umeanza Juni 8, 2023.

Habari Zifananazo

Back to top button