Rais Samia ateua mabalozi

RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi watatu kuwa na hadhi ya Balozi.
 
Katika uteuzi huo amemteua Dk Moses Kusiluka Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Balozi.
Pia, amemteua Dk Salim Othman Hamad Msaidizi wa Rais anayeshughulikia masuala ya siasa kuwa Balozi.

 
Aidha, amemteua Dk Kassim Mohamed Khamis, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia masuala ya Hotuba kuwa Balozi.
 
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, iliyotolewa leo Juni 13, 2023 inasema kuwa uteuzi huo wa hadhi ya balozi umeanza rasmi jana Juni 12,2023 na vyeo walivyonavyo vinabaki kama vilivyo.
 
Taarifa hiyo inasema kuwa wateule wote wataapishwa rasmi Juni 16 kuanzia saa nne kamili asubuhi, Ikulu Chamwino Dodoma.

Habari Zifananazo

Back to top button