“Tumempoteza kiongozi mahiri” -Samia

RAIS Samia Suluhu Hassan amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa.

“Mheshimiwa Lowassa ameitumikia nchi yetu katika nafasi mbalimbali kwa zaidi ya miaka 35, akianzia ushiriki wake katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge, Waziri katika wizara mbalimbali na Waziri Mkuu,”

Tumempoteza kiongozi mahiri, aliyejituma na kujitoa kwa nchi yetu. Natoa pole kwa mjane, Mama Regina Lowassa, watoto (Mheshimiwa Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa na wadogo zako), ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mzito”.ameandika Rais Samia kwenye mtandao wa X.

Advertisement

“Katika mawasiliano yangu na familia, nimewaeleza kuwa kama taifa tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu, na kamwe wasiache kumtegemea Mwenyezi Mungu na kutafakari neno lake, hasa Kitabu cha Ayubu 1:21. Mwenyezi Mungu amweke mahali pema. Amina.” Ameongeza.