Rais Samia atoa Sh milioni 10 kwa Twiga Stars

DAR ES SALAAM: RAIS,Samia Suluhu Hassan ameizawadia timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars kitita cha Sh milioni 10 baada ya timu hiyo kuisambaratisha timu ya Ivory Coast kwa Changamoto ya mikwaju ya penati katika kipute cha kuisaka tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika 2024.
Katika dakika 90 za Mchezo huo Twiga Stars imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 ushindi uliofanya matokeo ya jumla kuwa sare ya mabao mawili baada ya Ivory Coast kushinda mchezo wa juma lililopita wakiwa nyumbani.
Akitoa Taarifa hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema dhamira ya Rais Samia ni kuona Twiga Stars wanafuzu michuano ya Mataifa ya Afrika 2024.



