Rais Samia atunukiwa shahada ya heshima ya udaktari

RAIS Samia Suluhu Hassan ametunukiwa shahada ya udaktari wa heshima kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo wakati wa mahafali ya 52 duru ya 5.

Maazimio ya Seneti ya |Baraza la Chuo hicho yalipitishwa katika kiako cha 876 ambapo yalimpendekeza Rais Samia kutunukiwa digrii hiyo ya juu ya heshima ya falsafa kwa kile walichoeleza kuwa uongozi wa Rais Samia pamoja na mambo mengine ameleta mageuzi ya kiuchumi pia umeleta tumaini jipya.

Rais Samia amesemwa kuboresha elimu ikiwemo kujenga vyuo 25, kusaini na benki ya dunia mradi wenye thamani ya bililioni zaidi ya 900 wenye lengo la kuboresha elimu ya juu.

Rais Samia amemshukuru Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na baraza la seneti la chuo kikuu cha Dae es Salaam kwa kumpendekeza kupata tuzo hiyo na aliikubali kwa sababu siyo ya kwake pekee bali watanzania.

Rais Samia amesema alijaribu kutafuta shahada hiyo lakini muda haukumpa nafasi.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button