Rais Samia awasili London kushiriki maziko ya Malkia Elizabeth II

Rais Samia akiwasili London, Uingereza| Ikulu

RAIS Samia Suluhu Hassan amewasili jijini London, Uingereza kwa ajili ya kushiriki shughuli rasmi ya msiba wa Malkia Elizabeth II ambeya anatarajiwa kuzikwa Jumatatu, Septemba 19.

Rais Samia ataungana na viongozi mbalimbali walioalikwa kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu kwenye eneo la Westminster Hall ambapo pia atatia saini kitabu cha maombolezo, taarifa ya msemaji wa rais imesema.

Pia Rais Samia atahudhuria hafla fupi iliyoandaliwa na Mfalme Charles III pamoja na Mke wa Mfalme, Malkia Camila na imepangwa kufanyika katika Kasri ya Beckingham jijini London.

Advertisement