Rais Samia azindua mradi wa maji Kigamboni

Rais Samia akizindua mradi wa maji Kigamboni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusiana na mradi mkubwa wa maji ya visima 7 ambao unatoa maji zaidi ya lita milioni 70 kwa siku kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.

Advertisement

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuwasha mtambo (pampu) wa kusukuma maji kwenye tanki kubwa la maji kwa ajili ya usambazaji kwa wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.

 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuzindua Mradi wa maji Kigamboni ambao unatoa maji lita milioni 70 kwa siku kwa ajili ya wakazi wa maeneo mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni tarehe 11 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimkabidhi mfano wa ufunguo, Waziri wa Maji Jumaa Aweso pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga mara baada ya kuzindua na kugawa magari ya kuchimbia visima virefu na mabwawa sehemu mbalimbali nchini kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso pamoja na viongozi mbalimbali wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi na ugawaji wa magari ya mitambo kwa ajili ya kuchimbia visima virefu na mabwawa sehemu mbalimbali nchini kwenye hafla iliyofanyika Kigamboni Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuwasha mtambo (pampu) wa kusukuma maji kwenye tanki kubwa la maji kwa ajili ya usambazaji kwa wakazi wa maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2022.

1 comments

Comments are closed.