Rais Samia: Fedha bado zipo wekeni mipira wavuni

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezitaka timu za Simba na Yanga SC kuendelea kufunga mabao zaidi kwenye michezo ya kimataifa kwani fedha za kuwapa bado zipo.

Rais Samia amesema hayo leo Machi 19, 2023 wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka miwili ya utawala wake yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

“Niliona utani nampigia Msigwa, namwambia hebu maliza mpira haraka mimi pesa zimeisha, nataka niwahakikishie mama bado anazo wekeni mipira kwenye wavu, jengeni jina la nchi yetu bado zipo”.amesema Rais Samia.

Aidha Rais Samia amezipongeza timu hizo kwa kutumia fursa yake ya kununua goli moja kwa Sh 5,000,000 na kupelekea kufanya vizuri kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.

Amesema fursa hiyo inasaidia kuinua michezo nchini na kuzitaka timu hizo kuendelea kufanya vizuri katika michezo yao iliyobaki kwani fedha bado zipo na wataendelea kuzipata endapo watafunga kwenye michezo ijayo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button