Rais Samia kufungua kikao cha 77 haki za Binadamu

ARUSHA: RAIS, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua kikao cha 77 cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu kitakachofanyika Oktoba 20 hadi Novemba 9 ,mwaka huu Jijini Arusha.

Akizungumza katika kikao cha Mawaziri cha Kujadili Maandalizi ya Kikao hicho Jijini  Arusha Waziri wa Katiba na Sheria,Balozi Dk,Pindi Chana amesema maandalizi  yanakwenda vizuri na  wageni zaidi ya 700 kutoka mataifa mbalimbali watashiriki.

Advertisement

Balozi Chana amesema mbali na kujadili masuala ya msingi yanayohusu haki za binadamu lakini pia  watapata fursa ya kuitangaza nchi kwa mataifa mbalimbali juu ya utajiri na rasilimali zilizopo nchini.

Amesema masuala mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo maadhinisho ya siku ya haki za binadamu kwa kuzingatia,taarifa kuhusu hali ya haki za binadamu Barani Afrika,uzinduzi wa nyaraka mbalimbali za kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu,taarifa ya wanaharakati wa haki za binadamu,kuidhinishwa kwa itifaki ya mkataba wa Afrika wa Ulinzi wa Jamii.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *