Rais Samia kushuhudia viongozi Taasisi za Umma wakiteta

DAR ES SALAAM: Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Mkutano wa Viongozi wa Taasisi na Mashirika ya Umma unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha kuanzia Agosti 19 hadi 21 mwaka huu katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

Akitoa taarifa hiyo leo Agosti 13, 2023 Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesema Rais Samia atazindua rasmi mkutano huo wa kwanza wenye lengo la kuwakutanisha pamoja wakuu wa taasisi na mashirika ya umma ili kujadiliana kwa pamoja na kujua changamoto na mafanikio ya taasisi hizo.

Mchechu amesema katika kufikia dhamira ya kuwa na mashirika yanayojitegemea na kujiendendesha kwa faida wanakusudia kuja mabadiliko mbalimbali hasa ya kimuundo, sheria pamoja na kutoa uhuru kwa taasisi katika utendaji kazi.

“Tutangalia baadhi ya sheria labda zilizopitwa na wakati na kuangalia jinsi ya kuziboresha, kuhusu uhuru wa hizi taasisi tutawarudishia lakini tukiangalia jinsi ya utendaji wake, kwahiyo tunaamini kutakuwa na matumizi mazuri ya uhuru huo kwasababu tutakuwa tukifuatilia kwa ukaribu.”amesema Mchechu.

Aidha Msajili wa Hazina amesema kiu yake ni kuona taasisi zinaweza kujiendesha zenyewe na kuondokana na utegemezi kwa serikali huku zikifanya kazi zake kwa ufasaha.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Viongozi wa Taasisi za Umma Sabasaba Moshingi pamoja na makamu mwenyekiti wa Jukwaa hilo Latifa Hamisi wamesema Mkutano huo utajenga Jukwaa moja lenye maono ya pamoja ili kuijenga Tanzania inayotarajiwa na wapo tayari kulijenga Taifa imara .

Mkutano huo wa siku tatu utatumika pia kuzitambua taasisi zilizofanya vizuri katika utendaji wake ambapo zitatunzwa na kutoa mbinu za mafanikio kwa taaisi nyingine ili kuwa na mwelekeo mmoja huku kuanzia mwakani taasisi zitakzoshindwa kwenda na kasi inayotakiwa zikiwekwa hadharani.

Habari Zifananazo

Back to top button