Rais Samia mgeni rasmi maadhimisho ya JKT

RAIS Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa.

MKUU  wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema Rais Samia atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yatakayofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Julai 10, 2023.

Amesema maadhimisho hayo yatatanguliwa na maonesho mbali mbali  yatakayoanza Julai Mosi, 2023.

Ametaja maonesho yatakayotangulia ni ya vikundi vya sanaa na utamaduni pamoja na bidhaa zinazozalishwa na SUMAJKT, vikosi, shule na vyuo vya ufundi stadi vya JKT.

 

Habari Zifananazo

Back to top button