Rais Samia: |Sura zenu hamna dhamira ya kushika dola 2025

Asema wahafidhina wapo Chadema, CCM

RAIS  Samia Suluhu Hassan amesema kuwa hakuna sura za kushika dola kutoka upinzani na kwamba 2025 yeye yupo.

Rais Samia ameyasema hayo leo Machi 8, 2023  katika kongamano maalum la wanawake wa Chadema (|Bawacha) lililofanyika mkoani Kilimanjaro.

Amesema “Kwa sura ninazoziona hapa hamna dhamira ya kushika dola 2025 mnajua mama yupo, dhamira hiyo haipo.

“Wote mfanye siasa za kistarabu, katika kipindi kifupi nchi yetu inaheshimika duniani tusiirudishe nyuma, Tanzania ni taifa kubwa tusilitolee sifa yake” Amesema Rais Samia

Aidha, amesema kuna wahafidhina ndani ya Chadema kama ambavyo wapo pia CCM.

“Najua  Wakati nilipopendekeza kwenye chama changu tufungue mikutano wa adhara mjadala ulikuwa ni mkubwa, haikuwa rahisi, najua juzi Mbowe (Freeman) alikuwa na mjadala mkubwa sana kwa nini umemuita Rais kwenye mkutano wetu, kwa hiyo wahafidhina wapo wengi, kwenye chama chako, chama chetu.

“Najua unatandikwa umepewa asali umebadili  na ‘tone’, ulipotoka jela ulienda Ikulu mama alikwambia nini? ukienda nje unatandikwa…wahafidhina siku watatuelewa, asante ndugu yangu. (Mbowe) amesema Rais Samia

Rais Samia amesema Tanzania inajengwa na watanzania wenyewe na kutaka amani ijengwe ili mengine yafuate.

“Leo hapa tumejawa na furaha, na hiyo ni sababu ya matunda ya mazungumzo ya maridhiano ndugu zangu siasa ni mchezo wa kulumbana kwa hoja…..kasema nini nimzodoe, wote tukiwa na lengo la kushika dola.

“Mimi Dada yenu na wenzangu wanaonisaidia tumefanya ubunifu wa kuhakikisha Taifa hili linaungana na kuwa moja. Tukaviambia vyama vya siasa vikae na kuja na namna wanataka tufanye nini.”

“Katika hilo chama chenu kikaja na maoni yake ya kutaka kisikilizwe peke yake na mimi nikamwambia Makamu wangu awaite watu wenu watano na upande huu watano mambo yakasonga mbele.”

Baada ya vikao hivyo leo mnamuona Rais amesimama kwenye jukwaa hili kuzungumza na Baraza la Wanawake la CHADEMA, jambo ambalo halikuwa rahisi huko nyuma ila kwa sababu ya ubunifu limewezekana.”

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button