Rais Samia: Tumeboresha bajeti ya Mahakama

DODOMA :RAISĀ wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan amesema serikali imeboresha bajeti ya mahakama kutoka Sh bilioni 162.2 kwa mwaka 2021 mpaka kufikia Sh bilioni 321 kwa mwaka 25/26 lengo kuwe na huduma bora zenye tija na ufanisi .
Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati akifunga bunge la 12 na kusema kuwa ni sawa na ongezeko la asilimia 93
” Vilevile tumeongeza idadi ya majaji ,mahakimu na mawakili wa serikali na nafarijika kwamba tumezingatia uwakilishi wa kijinsia katika kipindi hiki pia nimeteuwa majaji wapya 83, ambapoa majaji wa mahakama ya rufani ni 15 kati yao 4 ni wanawake na majaji wa mahakama kuu 68 kati yao 30 ni wanawake.
” Tuliwezesha ajira mpya za mahakimu na watumishi wengine jumla 1,153 majaji na mahakimu wanawake wamekuwa wengi wakati huu kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi yetu,” amesema.
Samia amesema hatua hizo zimewezesha mahakama kufanya kazi kwa weledi na ufanisi pamoja na kuhakikisha mifumo ya tehama katika utoaji wa huduma za kisheria inasomana na mifumo na taasisi nyingine za sheria