Rais Trump kuapishwa leo

MAREKANI – RAIS Mteule wa Marekani, Donald Trump (78) anatarajia kuapishwa leo kuwa Rais wa 47 katika uapisho wa kihistoria nchini Marekani. Trump anaapishwa na kurejea tena Ikulu ya Marekani baada ya kukaa nje ya ofisi hiyo baada ya kushindwa katika uchaguzi wa 2017 uliomuweka madarakani Joe Biden.

Trump anakuwa rais wa pili kurejea madarakani baada ya kutolewa, wa kwanza ni Stephen Cleveland aliyekuwa Rais wa Awamu ya 22 na 24, aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 1885 hadi 1889 na kurejea tena 1893- 1897.

Trump anaingia madarakani akiwa na ajenda muhimu za kuimarisha uchumi wa Marekani huku akitazamiwa kuongoza juhudi za kumaliza vita ya Israel na Gaza na Urusi na Ukraine.

Kuhusu uhamiaji Trump aliahidi kuimarisha ulinzi kwa kujenga ukuta wa kuzuia wahamiaji kutoka nchi za nje kama Mexico na kuhamisha wahamiaji wasio na vibali. Katika uchumi Trump aliahidi kudhibiti mfumuko wa bei uliotokana na janga la Covid-19.

Pia, Trump aliahidi mageuzi katika kodi na kuongeza ushuru kwa bidhaa zinazotoka nje ya mipaka yao kutoka asilimia 10 hadi 20 lengo kuu ni kuimarisha biashara ambayo ilianza kudorora Marekani.

Trump aliwashinda wagombea wengine katika uchaguzi uliofanyika Novemba 5, 2024 kwa kupata kura 71,111,574 ambazo ni sawa na asilimia 51.2 akifuatiwa na Kamala aliyepata kura 66,180,612 sawa na asilimia 47.5.

Habari Zifananazo

Back to top button