Rais wa Burundi awasili Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Burundi, Évariste Ndayishimiye, amewasili jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).
Rais Ndayishimiye alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Hamza Hassan Juma, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Mkutano huu wa siku mbili umeanza kwa ngazi ya mawaziri, ukitarajiwa kufikia kilele chake leo Januari 28, ambapo Wakuu wa Nchi za Afrika watajadili mikakati ya kukabiliana na changamoto za nishati na kuchangamkia fursa zilizopo barani.

Matokeo muhimu yanayotarajiwa ni kupitishwa kwa Azimio la Dar es Salaam, linalolenga kuimarisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa maendeleo ya bara la Afrika.
RAIS WA GHABON AWASILI TANZANIA
Rais wa Gabon, Brice Oligui Nguema amewasili jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaofanyika nchini kuanzia leo Januari 27 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere.

Rais Nguema amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Mkutano huu unawakutanisha viongozi wa nchi za Afrika, wadau wa sekta ya nishati, na washirika wa maendeleo, ili kujadili mikakati na hatua za kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika.
RAIS WA GHANA AWASILI TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Ghana, John Dramani Mahama, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Mahama alikaribishwa na Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso.
Mkutano huu unawakutanisha viongozi wa nchi za Afrika, wadau wa sekta ya nishati, na washirika wa maendeleo, ili kujadili mikakati na hatua za kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika

RAIS WA ZAMBIA AWASILI TANZANIA
Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika.

Mkutano huu unawaleta pamoja Wakuu wa Nchi za Afrika, wataalamu wa nishati, viongozi wa sekta binafsi, na washirika wa maendeleo ili kujadili mikakati ya kukabiliana na changamoto na fursa za nishati barani Afrika.

Inatarajiwa kuwa mkutano huu utapitisha Azimio la Dar es Salaam, ambalo litasisitiza dhamira ya pamoja ya viongozi wa Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa ajili ya maendeleo ya bara la Afrika.
RAIS WA ETHIOPIA AWASILI TANZANIA
DAR ES SALAAM – Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Udemokrasia ya Ethiopia, Aye Atske Selassie, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika.
Mkutano huu unawaleta pamoja Wakuu wa Nchi za Afrika, wataalamu wa nishati, viongozi wa sekta binafsi, na washirika wa maendeleo ili kujadili mikakati ya kukabiliana na changamoto na fursa za nishati barani Afrika.
Inatarajiwa kuwa mkutano huu utapitisha Azimio la Dar es Salaam, ambalo litasisitiza dhamira ya pamoja ya viongozi wa Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa ajili ya maendeleo ya bara la Afrika.




