Rais wa Somalia anusurika shambulizi la bomu

MOGADISHU: Bomu lililotegwa kando ya barabara limelipuka jana nje ya kasri ya rais nchini Somalia, likilenga msafara wa rais.
Taarifa kutoka Wizara ya Mawasiliano imesema shambulizi hili la kighaidi linalodaiwa kupangwa na kundi la al-Shabab, wanaopinga utawala wa serikali ya shirikisho la Somalia. Hata hivyo, taarifa hiyo haikutaja idadi kamili ya wahanga wa bomu hilo.
Shuhuda mmoja alieleza kuwa aliona miili mitatu ya watu katika eneo la tukio, ingawa serikali haijathibitisha taarifa hiyo rasmi. Rais wa Somalia amenusurika na shambulio hilo, huku vikosi vya usalama vikiendelea kuchunguza tukio hili. SOMA: Samia akutana na Rais wa Somalia
Al-Shabab limekuwa likitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya serikali na wanajeshi wa Somalia, hasa katika maeneo ya Pembe ya Afrika, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kupinga utawala wa sasa.