Rais Yoon Suk agoma kuhojiwa na wachunguzi

KOREA KUSINI : RAIS wa Korea Kusini aliyeachishwa madaraka na bunge, Yoon Suk Yeol, amekataa kuhojiwa na wapelelezi baada ya kukamatwa kwa amri ya kutangaza sheria ya kijeshi.

Mahakama ya Kikatiba pia imeanza kikao cha pili cha kusikiliza kesi hiyo, ambapo itajadili kama itaruhusu uamuzi wa bunge wa kumvua madaraka Yoon au la.

Yoon, ambaye ni rais wa kwanza aliyeko madarakani nchini Korea Kusini kukamatwa na polisi, anakabiliwa na mashitaka ya uasi.

Katika mahojiano hayo, Yoon Suk alitumia haki yake ya kikatiba ya kukaa kimya kabla ya kuhamishiwa jela mjini Seoul. SOMA:Hatimaye Rais Yoon Suk akamatwa

Wapelelezi kutoka Ofisi ya Uchunguzi wa Rushwa walitarajiwa kuendelea kumhoji Yoon, lakini timu yake na mawakili wake waligoma kumhoji  Yoon kutokana na hali ya afya.

Wakati huo, maafisa wa sheria wanajaribu kupata waranti nyingine ili waweze kumshikilia Yoon kwa zaidi ya saa 48.

Habari Zifananazo

Back to top button