KOREA KUSINI : RAIS wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol, amekamatwa leo, na kuweka historia kama rais wa kwanza aliye madarakani kukamatwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mamlaka zinasema kuwa wachunguzi walilazimika kutumia ngazi kuingia katika makazi ya rais ili kumkamata baada ya kuwekewa vizuizi na wabunge wa chama tawala pamoja na mawakili wa Yoon.
Awali, wachunguzi walizuiliwa kwenye lango la kuingilia na magari yaliyokuwa yamewekwa kizuizi. SOMA: Vyombo vya usalama vyajipanga kumkamata Yoon Suk
Hata hivyo, baadhi ya wachunguzi walifanikiwa kufikia eneo hilo kwa njia nyingine ya kupanda mlima, na hivyo kuweza kuingia nyumbani kwa Yoon na kumkamata.
Wakati huo, waandamanaji walikusanyika kwenye makazi ya rais, wakishuhudia zoezi hilo la kukamatwa.
Hii ni hatua kubwa katika historia ya siasa za Korea Kusini, ambapo rais wa zamani amekamatwa kutokana na tuhuma za uasi.