Taji AGT kileleni ‘Paa la Afrika’

MOSHI, Kilimanjaro: WASHINDI wa Dunia wa Mashindano ya kusaka vipaji ya nchini Marekani ‘American Got Talent Fantasy League’ (AGT) ambao pia ni wasanii wa sarakasi nchini ‘Ramadhani Brothers’ wametimiza azma yao ya kufika katika kilele kirefu zaidi barani Afrika maarufu kama Paa la Afrika ‘Uhuru Peak’ uliopo katika Mlima Kilimanjaro.

http://RAMADHANI BROTHERS WASHINDA AGT, RAIS SAMIA APONGEZA

Lengo likiwa ni kutanganza Vivutio vya Utalii Tanzania pamoja na kampeni mahususi ya #VOTENOW katika kupigia kura Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Taifa Serengeti.

“Tumefanikiwa kuwasilisha tuzo yetu ya AGT katika kilele cha Afrika. Tumeishinda changamoto nyingine,” wameandika Ramadhani Brothers katika ukurasa wao wa mitandao ya kijamii wakijipongeza.

Ramadhani Brothers kileleni Kilimanjaro ‘Uhuru peak’

Kwa upande wao, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) wamewapongeza nyota hao wa sarakasi kwa kufanikisha safari hiyo kwa kushirikiana.

Habari Zifananazo

Back to top button