Ramaphosa achaguliwa muhula wa pili urais

AFRIKA KUSINI – KIONGOZI wa Chama cha African National Congress (ANC), Cyril Ramaphosa amechaguliwa kuhudumu kwa muhula wa pili kama rais wa Afrika Kusini.

Ramaphosa aliongoza kwa kupata kura 283 huku kiongozi wa Economic Freedom Fighters, Julius Malema akiambulia kura 44. Kura 12 ziliharibika.

Katika hotuba yake baada ya kuchaguliwa, alisema ana furaha na heshima kuendelea kutumikia taifa hilo kubwa katika nafasi ya rais. Ramaphosa alishukuru wajumbe wa Bunge la Kitaifa kwa kura zao.

Muungano kati ya ANC na kiongozi wa Democratic Alliance, John Steenhuisen umekuwa na mchango mkubwa katika kuchaguliwa kwa Ramaphosa kwenye nafasi hiyo kwa awamu ya pili.

Ramaphosa alitoa tangazo hilo juzi katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Cape Town (CTICC). Kiongozi wa Democratic Alliance, Steenhuisen alisema DA ilifikia makubaliano juu ya kauli ya dhamira ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Alisema DA na IF ya Wazulu itaunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa na kumuunga mkono Rais Ramaphosa katika uchaguzi wa urais.

Habari Zifananazo

Back to top button