KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Musa amewataka maofisa ugavi na manunuzi kuepuka kuzalisha hoja za ukaguzi zinazopelekea halmashauri kupata hati chafu ikiwemo kuzingatia vipengele vya mikataba ambavyo serikali inaingia kutokana na manunuzi kwenye miradi mbalimbali nchini.
“Lakini pia weledi na maadili ni msingi mkubwa katika kuhakikikisha miradi inatekelezwa ikiwa na viwango bora hivyo lazima eneo la manunuzi lingaliwe vizuri na ikibainika kinaukiukwaji wa sheria wahusika watachukuliwa hatua za kinidhamu,”
Musa ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kwaajili ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi kutoka taasisi mbalimbali za Mkoa wa Arusha ikiwemo mfumo wa Kieletroniki wa Ununuzi wa Umma(Nest) ililoshirikisha wataalam hao zaidi ya 120.
Amesema ufanyaji kazi kwa weledi na maadili kwa kutendea haki kwani fedha zinazotolewa na Rais Samia Hassan Suluhu kwenye miradi mbalimbali ni nyingi hivyo misingi ya taaluma za ununuzi lazima itendewe haki kwa faida ya kizazi kijacho.
Amesisitiza matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa Ununuzi wa Umma( NeST) kwani mfumo huo sio kichaka cha wizi bali unadhibiti wizi kutokana na kufanya manunuzi kupitia
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema hivi karibuni bodi hiyo ilifanya ukaguzi kwenye maeneo mbalimbali na kubaini kunabaadhi ya maofisa manunuzi na ugavi hawasajiliwa na bodi hiyona kusisitiza ni vema wakafuata sheria ili wasije kumbana na adhabu.