MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella ameliagiza Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kuhakikisha hoja zao hazijirudii wakati wa usilishaji wa hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye mkutano wa baraza la maalum la madiwani wa halmashauri hiyo la kupitia na kujadili majibu ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za mwaka wa fedha 2021/2022.
Amesema ni vyema madiwani hao kupitia taarifa na kutoa ufafunuzi wa hoja zilizoibuliwa ili ziweze kufutwa au kupatiwa mujibu mbapo amewataka madiwani hao kuhakikisha hoja zinazowasilishwa hazijirudii.
Ameongeza kuwa usimamizi makini ukiwepo kwenye kila kitengo na idara kutarahisisha uwepo wa hoja chache na makini,zisizojirudia ambapo amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kuwajibika kwa wananchi kwa kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye kata zao inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.
Sanjari na hilo ameipongeza halmashauri hiyo kwa kupata hati inayoridhisha ambapo amewataka pia kuendelea kuondoa changamoto ndogondogo zilizopo ili kuifanya halmashauri kukua kimaendeleo na kuwasisitiza madiwani kuwajibika na kusimamia miradi yote inayotekelezwa kupitia fedha mbalimbali ikiwemo fedha Mradi wa Kuimarisha ufundishaji na Ujifunzaji kwa shule za Awali na Msingi Tanzania Bara ( BOOST).