RC Dar azindua mfumo usambazaji gesi ya LPG

DAR ES SALAAM;MFUMO wa kwanza wa usambazaji wa gesi ya LPG kwa wingi katika Soko la Samaki Feri Dar es Salaam umezinduliwa rasmi.

Mfumo huo nisehemu ya mkakati wa kuimarisha upatikanaji wa nishati safi nchini, ambapo Kampuni ya ORYX Energies Tanzania imezindua mfumo huo kwa kushirikiana na serikali na wadau wa soko.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila uzinduzi huo ni mabadiliko ya kweli katika usalama, ufanisi, na ustawi wa kila mfanyabiashara Soko la Feri.

Alisema Oryx wameweka miundombinu mizuri na mtandao wa mabomba unaohudumia majiko yote 48 na kwamba kila mfanyabiashara atakuwa na mita yake inayosoma matumizi yake ya kila siku, kabla na baada ya matumizi.

Mradi huo wa ubunifu umetajwa kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya nishati ya kupikia nchini, hasa kwa wafanyabiashara wadogo na mama lishe wanaotumia gesi kwa shughuli zao za kila siku.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Tanzania, Araman Benoit mradi huo umegharimu zaidi ya Sh milioni 250 kwa ufadhili wa asilimia 100 kutoka Oryx Energies.

Amesema mfumo huo unatumia teknolojia ya kisasa ya malipo kwa kutumia mita ya kulipia kadri ya matumizi (LUKU), hivyo kuondoa hitaji la kununua mitungi mikubwa au midogo ya gesi, na kupunguza gharama kubwa walizokuwa wakizilipa awali

Amesema wafanyabiashara waliokuwa wakitumia hadi Sh 180,000 sasa wataokoa Sh 45,000 kwa siku kupitia mfumo wa LUKU, jambo linalowasaidia kupanga bajeti zao kwa ufanisi zaidi.

Pia amesema mfumo umeondoa changamoto ya mitungi kuisha ghafla wakati wa shughuli za kupikia, kwani gesi hupatikana moja kwa moja kupitia bomba kutoka kwenye tangi kubwa lililofukiwa ardhini.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Kamishna wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati, Innocent Luoga aliipongeza Oryx kwa kuunga mkono jitihada za serikali kupitia Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024/2034.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amepongeza teknolojia hiyo na kwamba imekuja wakati sahihi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button