RC Kagera ataka watendaji washirikiane

MKUU mpya wa Mkoa wa Kagera, Fatuma Mwasa amefanya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Albert Chalamila aliyehamishiwa Mkoa wa Dare es Salaam na kutaka watendaji wafanye kazi kwa ushirikiano.

Fatuma Mwasa anaandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika historia ya mkoa huo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi, Mwasa alisema anatambua mkoa huo upo mpakani na waliopita wengi ni wanaume na wanajeshi, hivyo anajivunia kufungua historia ya kuwa  mwanamke wa kwanza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, huku akiwataka watendaji wote mkoani Kagera wanafanya kazi kwa ushirikiano .

“Naomba niwahakikishie kuwa kama Chalamila alivyoondoka mkalia mkahuzunika, mkaandika mengi mtandaoni, ndivyo ambavyo siku nikija kutoka Kagera itakuwa, kwa sababu kwa upande wangu hakuna maneno ni kazi kazi na hakuna tofauti na kazi, “alisema Mwasa.

Alisema kuwa anaanini mkoa huo unamdai kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ambayo wananchi wake wanashauku kubwa itekelezwe, hivyo anaamini itatekelezwa haraka, kwa viwango vizuri.

Alisema Mkoa wa Kagera utaendelea kuwa na kipato kizuri, ili kuchangia pato la Taifa  pamoja na kukuza pato la mtu mmoja mmoja kupitia kilimo na ufugaji.

Kwa upande wake Chalamila katika makabidhiano hayo, alisema kuwa  mkuu huyo wa mkoa asiogope kutekeleza majukumu yake kwa sababu ya maneno ya watu wachache, badala yake afanye kazi kubwa ya kuisaidia jamii kuhakikisha anatekeleza miradi yote inayoletwa na serikali.

Habari Zifananazo

Back to top button