RC Mtanda: Miradi ya Trilioni 5.6 yatekelezwa Mwanza

MWANZA : WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kitaifa la ufuatiliaji, tathmini na kujifunza, litakalofanyika jijini Mwanza kuanzia kesho Septemba 10 hadi 13, 2025.
Akizungumza na waandishi mjini Mwanza , Mtanda amesema ufuatiliaji ni silaha muhimu kwa serikali katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati, kwa ubora na kwa thamani halisi ya fedha. “Kupitia ufuatiliaji na tathmini inayofanyika mara kwa mara kumewezesha utekelezaji wa miradi yenye thamani ya Sh trilioni 5.6 mkoani Mwanza, iliyotolewa na serikali kuu kuanzia mwaka 2021 hadi 2025,” alisema.
Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na Daraja la John Pombe Magufuli, meli ya MV Mwanza, vivuko vipya, hospitali ya hadhi ya kutoa huduma za kibingwa wilayani Ukerewe, soko kuu la kisasa na kipande cha reli ya kisasa cha Mwanza–Kahama. Hatahivyo amesema kongamano hilo litakutanisha washiriki 1,000 kutoka ndani na nje ya Tanzania. SOMA: Naibu Waziri Byabato atoa maelekezo Miradi Mwanza



