RC Mtwara akabidhi magari ya wagonjwa 10 Mtwara

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amekabidhi magari 10 kwa sekta ya afya katika baadhi ya halmashauri mkoani humo yatayotumika katika shughuli mbalimbali za kiutendaji ikiwemo kubebea wagonjwa.

Mgari hayo yamekabidhiwa kwa baadhi ya wabunge kutoka majimbo mbalimbali mkoani humo ikiwemo Mtwara Mjini, Mtwara Vijijini, Nanyamba, Masasi Vijijini na Newala.

Akizungumza wakati wa ghafla hiyo, mkuu huyo wa mkoa amesisitiza na kutoa rai kwa wataalam wanaokabidhiwa vitendea kazi hivyo.

Advertisement

‘’Lazima kuyafanyia sevisi kinyume na hapo yanaweza yakagharimu fedha nyingi au kutotumika moja kwa moja kwahiyo tujitahidi katika swala hili.’’amesema Abbas

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Bahati Geuzye amesema katika magari hayo yaliyokabidhiwa matano yatatumika kubeba wagonjwa na mengine matano shughuli za usimamizi na ufuatiliaji.

Awali mkoa huo ulikuwa na magari manane ya kubeba wagonjwa ambapo mengine yalikuwa mabovu na sehemu zingine hazikuwa na magari kabisa.

Kupitia jitihada za serikali ndani ya mwaka mmoja imeshaleta magari 12 hivyo kupelekea kuwa na magari 20 sawa na ongezeko la magari 12.

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota ‘’Nilikuwa na upungufu wa magari ya kubebea wagonjwa, magari haya sasa yanaenda kutatua hiyo changamoto hii’’amesema

Mkuu wa Wilaya ya Newala Rajabu Kundya ameipongeza serikali kwa kuwasaidia nyezo zitazowezesha wananchi wao kupata huduma bora za afya.

Hata hivyo watumishi wa umma kuwatumikia vizuri zaidi wananchi na kuhakikisha wanakuwa na nguvu za mwili, akili na kuweza kuzalisha mali kadri wanavyoweza.

Katika hatua nyingine pikipiki 5 zimegawiwa kwa maofisa ugani mifugo wa halmashauri ya Wilaya ya Mtwara katika ghafla hiyo.